Saturday, July 27, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya

YAFAHAMU MAZOEZI 10 BORA SANA KWA AJILI YA KUPUNGUA UZITO

Kama unasoma makala hii huenda wewe ni mdau wa mazoezi na fitness au una nia ya kupunguza uzito hivyo makala kama hizi zinakuvutia.
Pamoja kwamba ulaji wa chakula unachangia sana mtu kupungua uzito, mazoezi pia yana nafasi yake katika kupungua uzito na kukupa muonekano bomba.
Unaweza kupungua kwa chakula tu lakini utakua kama umekonda yaani hautakua na muonekano mzuri kama mtu ambaye kapungua kwa chakula na mazoezi.

Female runner running at summer park trail . Healthy fitness woman jogging outdoors.

Kuna mazoezi mengi sana ya kupungua uzito na yote yanafanya kazi lakini yanatofautina kasi ya kupungua uzito.
watu wengi wanaamini mazoezi ya kukimbia au aerobic yanapunguza uzito haraka ni kweli yanachoma mafuta hapo hapo lakini mazoezi ya kubeba uzito yanaendelea kukupunguza uzito masaa mpaka siku baada ya mazoezi hayo.
Leo tutaangalia mazoezi kumi ambayo ynapunguza uzito haraka kulingana na wingi wa calories au uzito kumbuka calorie 7700 ni sawasawa na kilo moja ya uzito na upunguaji hutegemea na uzito yaani mtu mwenye uzito mkubwa anachoma calories nyingi kwa kufanya mazoezi sawa na mtu mwenye uzito mdogo.
kubeba chuma; haya ni mazoezi ambayo sio hupunguza tu uzito lakini hujenga na misuli pia na kama nilivyosema hapo mwanzo mazoezi haya huchoma calories 250 mpaka 300 kwa saa lakini kwasaabu shughuli ya kuendelea kuchoma huendelea hata ukiwa ushatoka mazoezini ni kwamba unaweza kuchoma zaidi sababu yaani kesho yake 200, kesho kutwa 100 na kadhalika kwani mwili wako utaendelea kuhitaji oygen nyingi kwa ajili ya misuli hiyo.

kuruka kamba:Ni zoezi ambalo unaweza kulifanya kwenye mazingira yeyote hata kama kuna hali mbaya ya hewa na kifaa chako ni kamba tu na eneo la kurukia..inaweza kua chumbani au sebuleni.
kwa kasi ya kuruka mara 120 kwa kwa dakika unaweza kuchoma calories 667 mpaka 990 kwa saa kulingana na uzito wako.

kukimbia kupanda mlima; ukifanya mazoezi ya kukimbia na kupanda mlima yanachoma mafuta zaidi kuliko kukimbia kawaida kwenye mstari ulionyooka au tumambalale.
kwa kupanda mlima na kushuka unaweza kuchoma calories 639 mpaka 946 kulingana na uzito wako.

mazoezi ya kupigana au kick boxing; sio mazoezi ya watu wengi hasa hap kwetu kwasababu ni mchezo ambao unachukuliwa kwamba ni wa ugomvi tu lakini wanaofanya mazoezi haya huchoma calories 582 mpaka 864.

kuendesha baiskeli; kuendesha baiskeli hasa maeneo yenye muinuko kidogo huku ukichochea kwa kasi sana kunachoma mafuta zaidi kuliko kuendesha taratibu sehemu zenye miteremko.
mazoezi haya yanakadiliwa kuchoma calories 568 mpaka 841.

kukimbia tambalale; mazoezi ya kukimbia uwanjani au mtaani ni moja ya mazoezi pendwa na watu wengi, na yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupungua na kua fit.
mazoezi haya yanakadiriwa kuchoma calories 566 mpaka 839 ukikimbia umbali wa kilometa 16 ndani ya saa moja kwa mwendo wa kawaida japokua ukikimbia kwa kasi zaidi unachoma zaidi.

mashine ya baiskeli; hii ni ile baiskeli ambayo ni maalumu kwa ajili ya mazoezi, huweza kutumika sehemu yeyote na kukupa majibu mazuri.
naweza kuchoma calories 498 mpaka 738 kama ukiendesha kwa kasi ndani ya saa moja, kumbuka kuongeza ugumu wa baiskeli kwa matokeo chanya zaidi.

mazoezi ya kupanda ngazi; ni mazoezi mazuri hasa kwa watu ambao wanaishi sehemu zenye maghorofa au viwanja vikubwa , unaweza kuamua usitumie lift mara moja moja ukitoka kazini na kupanda kwa ngazi mpaka nyumbani kwako.
mazoezi haya huchoma caories 452 mpaka 670 kwa kila ngazi 77 unazozopanda hasa ukiwa kwa mwendo wa haraka.

Fitness woman she is running up the stairs.

planking; haya ni mazoezi ya kukunja mikono kama unalala chini kisha unabaki hivohivo kwa muda fulani mpaka unapochoka na kuachia, zoezi hili ni gumu kidogo lakini unaweza kufanya muda mwingi zaidi kadri unavyozoe na hukadiriwa kuchoma calories 4 mpaka 5 kwa dakika.


mwisho; haya ni mazoezi ambayo unaweza kuyafanya kama unataka kupungua haraka lakini kama wewe ni mnene sana au una sababu za kiafya za kushindwa mazoezi haya unaweza ukaanza kwa kutembea kwanza kwani mazoezi ya kutembea pia yana uwezo wa kumpunguza mtu na kumpa afya njema.
STAY ALIVE

DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO (MD)
0653095635/0769846183

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *