Friday, April 12, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya ya AkiliAfya ya uzazi

FAHAMU TATIZO LA MWANAMKE KUA NA UKE MKAVU NA MATIBABU YAKE

Tatizo la uke mkavu lipo kwa baadhi ya wanawake japo sio wote, ni tatizo ambalo kimsingi linaweza kuleta msongo wa mawazo kwa wahusika, maumivu wakati wa tendo ndoa,kukosa hamu ya tendo la ndoa,au kuvunja mahusiano kabisa, kupata vidonda ukeni hata kuvuja damu.
Ni tatizo ambalo linaweza kua chanzo cha aibu kwa wanawake na kushindwa kujieleza tatizo hilo kwa wataalamu wa afya kwa kuogopa aibu.

Kushuka kwa kiwango cha homoni ya oestrogen mwilini hasa mwanamke anapofikisha umri wa miaka 40 kwenda mbele ndio chanzo kikuu cha kukauka kwa uke na dalili hizo hua wazi kabisa mwanamke anapofikika menopause au mwisho wa kuona siku zake za mwezi lakini kuna vyanzo vingine kama
msongo wa mawazo
kunyonyesha
kuvuta sigara
baadhi ya magonjwa mfano hypothyrodism
mazoezi makali
uzazi
matibabu ya saratani
upasuaji wa kuondoa mayai ya mama.
baadhi ya dawa
kutokua na hisia na mwenza husika.
Nini cha kufanya?
ukipata tatizo hili unaweza ukamuona mtaalamu wa afya ambaye atakuchukua maelezo marefu na baadae atakupa suluhisho la matatizo yako kulingana na chanzo ambacho atakiona.
Lakini pia kwa wanawake ambao wanapata ukavu huu sababu ya umri basi kuna dawa mbalimbali za kupaka ambazo hua zina homoni ya oestrogen ndani yake ambayo huweza kusaidia tatizo hili, kumbuka tumia dawa tu ambayo imeelekezwa kwa kazi hii kwani baadhi ya dawa zimechanganywa na vitu mbalimbali kama perfume, na vitu asilia ambavyo sio salama kwa uke.

STAY ALIVE

DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO(MD)
0653095635/0769846183

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *