Saturday, July 27, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya ya uzazi

UFAHAMU UGONWA WA TEZI DUME NA MATIBABU YAKE

Tezi dume ni nini?
Huu ni ugonjwa unaotokea baada ya kuvimba kwa tezi inayofahamika kwa jina la prostate gland, tezi hii huanza kuvimba mwanaume anapofikisha miaka arobaini na kuendelea na tafiti zinaonyesha kwamba nusu ya wanaume wa miaka 50 na kuendelea wana tatizo hili.

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
Homoni za kiume; homoni maarufu kwa jina la testosterone ni homoni ambazo humfanya mtu aitwe mwanaume kwanzia kubalehe, uzazi wa mwanaume na muonekano wake.
Tafiti zinaonyesha kwamba homoni hii ni moja ya chanzo kikuu kwani wanaume ambao wana tatizo hili kwani wanaume ambao waliondolewa korodani walionyesha kutougua ugonjwa huu.
chakula; Tafiti zinaonyesha kuna mahusiano kati ya aina vya chakula na ugonjwa huu, watu wanaoishi mjini na kula nyama kwa wingi huathirika zaidi kuliko wale ambao wanakula vyakula vya ambavyo vina protini kidogo maeneo ya vijijini.
umri; kuna misuli ambayo inazuguka tezi dume muda wote, umri unavyozidi kwenda basi misuli ile inazidi kuchoka na kuipa nafasi tezi hiyo kuvimba.

dalili za ugonjwa huu.
kukojoa mara kwa mara
kuamka usiku kukojoa mara kwa mara
kushindwa kuzia mkojo ukibana
kujikojolea usiku
maumivu wakati wa kukojoa
jinsi ya kugundua tatizo hili
Tatizo hili linaweza kugunduliwa kwa historia ya mgonjwa, ukaguzi wa kitaalamu au physical examination na kuchukua baadhi ya vipimo.
kipimo cha utrasound huweza kugundua tatizo husika kupima ni kiasi gani tezi hiyo imeongezeka kwa ukubwa.
Vipimo vingine huchukuliwa kuangalia magonjwa ambayo yameambatana, yanafanana au yameletwa na ugonjwa huu mfano ni kipimo cha sukari, kipimo cha uwezo wa figo kufanya kazi na kipimo cha satatani ya tezi dume kitaalamu kama PSA.

matibabu;
matibabu ya tezi dume yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, kuna matibabu ya dawa na matibabu ya upasuaji.
mgonjwa kwa mara ya kwanza utatibiwa na dawa kama finastreride, doxazosin, terazosin na kadhalika na pia atawekewa mpira wa kuondoa mkojo kama atashindwa kukojoa vizuri.
Lakini kama matibabu haya yasipofanya kazi nzuri basi mgonjwa huyu atafanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi hiyo.

Aina hizi za upasuaji zimegawanyika katika sehemu mbalimbali kutokana na teknolojia inayotumika sehemu husika.
Madhara ya upasuaji ni kama kutokwa damu nyingi, kushindwa kutoa mbegu, kuishiwa nguvu za kiume na kuumia kwa njia ya mkojo.

STAY ALIVE

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *