Saturday, December 7, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Magonjwa

UFAHAMU UGONJWA WA MOYO WA ATRIAL FIBRILLATION NA MATIBABU YAKE

Atrial fribrillation ni ugonjwa wa moyo ambao unasababishwa na hitilafu ya mfumo wa umeme kwenye chemba za juu za moyo kitaalamu kama atrium. Ugonjwa huu husababisha moyo kutodunda kwa mtiririko sahihi hivyo damu kutoka kwenye moyo kushindwa kusambaa vizuri kwenda kwenye chemba za chini za moyo na pia kushindwa kwenda kwenye mwili mzima. Mara nyingi waathirika ni watu wa umri zaidi ya miaka 60 lakini unaweza kutokea kwa umri wowote ule.

Mkanganyiko huu wa damu unaweza kusababisha damu kuganda na kutengeneza mabonge ambayo. huweza kwenda kwenye ubongo na kusababisha kiharusi. ugonjwa huu huweza kuja na kuondoka au ukawa wa kudumu. Bila matibabu ugonjwa huu unaweza kusababisha kifo lakini kwa matibabu sahihi mgonjwa huweza kuishi maisha ya kawaida kama wengine.

Chanzo cha ugonjwa.

Chanzo cha ugonjwa huu hua hakifahamiki mara zote lakini hatari za kupata ugonjwa huu ni kama zifuatazo;

shinikizo la damu
upasuaji wa moyo
matumizi ya baadhi ya dawa mfano ibuprofen.
kuzaliwa na moyo wenye matatizo
unene wa kupindukia
ulevi wa kupindukia
umri mkubwa
historia ya ugonjwa huu kwenye ukoo.
magonjwa ya mapafu.
uvutaji wa sigara.

Jinsi ya kutambua ugonjwa..
Daktari anaweza kutambua ugonjwa huu kirahisi kwa kusikiliza mapigo ya moyo lakini pia kuna vipimo ambavyo huchukuliwa kama ECG,ECHO,UTRASOUND na baadhi ya vipimo vya damu hufanyika kuangalia chanzo na madhara ambayo yanaweza kua tayari yameababishwa na ugonjwa huu kama X RAY, D dimer, na kadhalika.

Matibabu ya ugonjwa huu.

Mwanzoni mgonjwa hutibiwa na dawa mbalimbali za moyo ambazo huhusika kuuweka moyo sawa ili uweze kwenda vizuri, dawa hizo ni kama digoxin,nifedine, poropanol na kadhalika lakini pia mgonjwa hupewa dawa za kuzuia damu kuganda kuweza kuzuia kiharusi.
Kwa baadhi ya wagonjwa matibabu haya yanaweza yasiwasaidie sana hivyo upasuaji huweza kufanyika kurekebisha tatizo hili japokua sio suluhisho la kudumu.

jinsi ya kuzuia ugonjwa huu.
Baadhi ya watu ambao wanatoka kwenye ukoo wa au familia yenye ugonjwa huu hawawezi kujizuia lakini atu wengine wanaweza kujizuia na ugonjwa huu kwa kupunguza uzito, kunywa pombe kiasi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kuacha sigara, na kutumia dawa vizuri kwa wagonjwa wa presha na kisukari.

 

STAY ALIVE

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *