Wednesday, July 24, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya ya uzazi

SABABU 3 ZINAZOONYESHA KWAMBA WATOTO WOTE WA KIUME WALIKUA WA KIKE KWANZA TUMBONI.

Wakati mwingine ukweli ni mchungu lakini hakuna uchungu kamtania mwanaume kuhusu jinsia yake lakini ukweli utabaki kwamba kila binadamu tumboni huanza kama mwanamke. Mtoto wa kiume akiwa tumboni kwa mama yake kabla ya wiki ya saba anakua ashaanza kupata maumbile ya kike, hivyo ni homoni za kiume ambazo zikiingilia kati zinamfanya abadilike kua wa kiume lakini kama homoni za kiume zisipoingilia kati basi anaendelea na kuzaliwa kama mtoto wa kike.Kwa lugha nyepesi ni kwamba wanaume wote waliwahi kua wanawake hapo zamani na bila homoni ya testosterone wangeendeelea kua wanawake na kuzaliwa na jinsia hiyo. Na ufuatao ni ushahidi kwamba wanaume wote hao walikua wakike mwanzoni.

Matiti kifuani; Matiti yanatengenezwa mapema sana kipindi cha ukuaji wa mtoto tumboni lakini kwa wanaume ni kama mapambo tu kwani hayana kazi yeyeyote. Hivyo kwa matiti ambayo wanaume wanayo kama wangepitiwa na homoni za kike sasa hivi wangekua wanatoa maziwa mengi tu na konyonyesha kama wanawake.

Uume; wakati wa ukuaji tumboni, homoni mbili yaani Mullerian inhibiting substance na dihydrosterone hutengenezwa kwa wanaume na kuleta uume lakini bila homoni ile uume huo ungebaki kama kinembe tu cha kwenye mwili wa mwanamke.

mstari wa kutoka kwenye korodani kwenda kwenye njia ya haja kubwa; Mstari huu kitaalamu uniatwa raphae line, kipindi cha ukuaji tumboni kila mtu ana uwazi sehemu ya viungo vya uzazi na bila homoni za kiume uwazi ule hutengeneza uke na viungo vya uzazi vya mwanamke lakini homoni za kiume hufanya ile sehemu kufunga na kuacha mstari kama kovu ambao ni kumbukumbu kwako kwamba ulitaka kua mwanamke kipindi fulani.

STAY ALIVE

DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

0769846183/0653095635

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *