DAWA YA UKIMWI (ARV) YA SINDANO MOJA KWA MWEZI YAANZA KUTUMIKA MAREKANI NA ULAYA.
Baada ya tafiti za muda mrefu ili kuwapunguzia mzigo wa dawa watumiaji wa dawa za virusi vya ukimwi ambao wengi wamekua wakilalamika kuhusu kuchoshwa na umezaji wa dawa hizo kwa muda mrefu basi wanasayansi wameweza kuja na dawa ya ARV ya sindano ambayo inayochomwa mara moja kwa mwezi, na kwasasa dawa inayochomwa ni mchanganyiko wa cabotegravir rilpivirine
ubora wa dawa hii ukoje?
Tafiti mbili zilifanyika ambapo watu ambao ni wagonjwa wa muda mrefu walisimamishwa dawa za kumeza na kuanzishiwa dawa ya sindano lakini pia tafiti nyingine ilifanyika ambayo wagonjwa wapya wa ukimwi walianzishiwa dawa hii na matokeo yalionyesha kwamba dawa zote mbili zilikua na matokeo mazuri kwenye kufubaza virusi vya ukimwi.
je ina madhara gani?
Mpaka sasa hakuna madhara yeyote ambayo yametangazwa kuhusu dawa hii zaidi ya maumivu wakati wa kuchoma sindano kitu ambacho ni kawaida kwa aina zote za sindano.
Je dawa hii inapatikana Tanzania?
Mpka sasa dawa hii haijaanza kutumika nchini Tanzania, lakini imekubaliwa na kuanza kutumika nchini canda, marekani na nchi zote za ulaya na mpaka sasa hivi hakuna anyejua dawa hizo zitafika huku kwetu lini.
Inatumikaje?
Kama nilivyosema hapo mwanzo mgonjwa atakua anachoma sindano moja tu kila mwezi badala ya vidonge lakini pia kwa watu ambao wanataka kujikinga na ugonjwa wa ukimwi pia wanaweza kuchoma sindano hii mwezi kabla na kushiriki tendo bila kua na hatari ya kuambukizwa.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE
0769846183/0653095635