Monday, September 9, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya

FAHAMU SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA KIFO WAKATI WA TENDO LA NDOA.

Hivi karibuni kumekua na ongezeko la vifo vingi vya watu hasa wanaume kwenye nyumba za kulala wageni ambapo inasemekana kwamba vifo hivo vilitokea wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Kumekua na hofu na imani za kishirikina kwamba huenda watu hao wamerogwa au wametegewa kitu cha kishirikina ndio maana wamekufa lakini mambo yote hayo hayana ushahidi.

Kitaalamu kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kuleta kifo wakati wa tendo la ndoa na mara nyingi huhusisha mfumo wa moyo kama ifuatavyo.

Magonjwa ya moyo; kuna wachezaji kadhaa wameshawahi kufia uwanjani wakati wa kucheza mpira, vifo hivi havina tofauti na vifo ambavyo vinatokea wakati wa tendo la ndoa.

Magonjwa ya moyo kitaalamu kama cardiomyopathies ndio yanayoongoza kwa vifo vya ghafla kwa vijana mpaka watu wazima hasa wakati wa mazoezi makali, magonjwa haya huja na kuvimba sehemu za ndani au chemba za moyo na kufanya ubadilishaji wa damu kutoka kwenye moyo kwenda sehemu zingine za mwili kua mgumu sana.

Vyanzo vya magonjwa haya hua ni kurithi kwa mzazi mmoja, ulevi wa kupitiliza, kuugua presha kwa muda mrefu, unene na magonjwa ya sukari,matumizi ya baadhi dawa za saratani,madhara ya ujauzito, madawa ya kulevya kama cocaine na kadhalika.

Dalili za magonjwa haya ni kuumwa kifua, kupumua kwa shida na kufa ghafla, mara nyingi magonjwa haya yanakua hayana dalili kabisa na mtu anaweza kukutwa na ugonjwa huu wakati wa vipimo vingine vya magonjwa mengine au uchunguzi baada ya kifo cha ghafla.

Magonjwa haya hayatibiki kabisa lakini kuna dawa malimbali za kupunguza makali au kubadilisha moyo kwa watu wenye uwezo huo.

dawa za kuongeza nguvu za kiume; Dawa maarufu kabisa inayotumika kutibu nguvu za kiume ni viagra kitaalamu kama sedenafil citrate, dawa hii inatakiwa iandikwe na kutumika chini ya uangalizi wa daktari na kwa lugha rahisi sio kila mtu anafaa kutumia dawa hii.

Viagra inafanya kazi kwa kutanua mishipa ya mwili ili kusukuma damu nyingi sana kwenye uume lakini faida hii inaambatana na madhara ya kushuka kwa presha ya damu, kitu hiki ni hatari sana kwa watu wenye presha ya kushuka na magonjwa mbali mbali ya moyo kwani hawezi kuvumilia tatizo hili na huweza kupelekea kifo cha ghafla kwa muhusika.

Kabla ya kutumia dawa hizi ni vizuri kuonana na wataalamu kwa ajili ya vipimo mbalimbali na kama wewe ni mgonjwa wa moyo tayari ni vizuri kukaa mbali kabisa na dawa hizi.

mwisho; Kila kitu kina wakati wake, kama wewe ni kijana na una uhakika una afya njema unaweza kufanya haya mashindano ya ngono lakini kama afya yako haiko sawa au umri umeenda sana basi kubali yaishe na ushiriki tendo hili kwa kiasi.Hakuna mtu amewahi kushinda chochote kwa kuonyesha umwamba wakati wa tendo la ndoa.

Maumivu ya sehemu ya moyo na kushindwa kupumua wakati wa tendo la ndoa inaweza kua dalili ya kwanza ya kuelekea kusimama kwa moyo, ukifika hatua hii usiendelee na omba msaada wa haraka kwani muda wowote unaanguka.

STAY ALIVE

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *