Wednesday, July 24, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya ya uzazi

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA UUME NA MATIBABU YAKE

Saratani ya uume ni ugonjwa adimu kidogo lakini hua unatokea, saratani hii huweza kutokea sehemu yeyote kwenye uume lakini mara nyingi hutokea kwenye kichwa cha uume au kwenye ngozi ya mbele ya uume au govi kwa mtu ambaye hajatahiriwa au hutokea ndani ya mishipa ya damu ya uume..

Wataalamu hawajui chanzo cha uhakika wa saratani hii lakini lakini kuna mambo ambayo huleta hatari ya kupata ugonjwa huu kama..

Ugonjwa wa zinaa wa Human papiloma virus.
Kuvuta sigara
Ugonjwa wa ukimwi
Umri zaidi ya miaka 60
Mtu ambaye hajatahiriwa.
Dalili za saratani hii ni kama zifuatazo.
Kubadilika kwa unene na rangi ya ngozi.
Vipele kwenye uume.
Uvimbe kwenye uume.
Harufu mbaya chini ya ngozi kwa watu ambao hawajatahiliwa.
kidonda kwenye uume ambacho kinavuja damu kirahisi.

Jinsi ya kutambua ugonjwa hospitali.
Sampuli ya uvimbe wa kwenye uume huchukuliwa na kwenda kupimwa maabara kuangalia kama kweli uvimbe huo ni saratani lakini pia vipimo vingine vya mionzo kama CT scan, utrasound, x ray na MRI hufanyika kuangalia saratani imesambaa kiasi gani mwilini.

Matibabu ya saratani ya uume
Matibabu ya saratani ya uume hutegemea hatua ambayo saratani imefika na katika hatua za mwanzo kabisa kuna cream za kutumia, matibabu ya barafu kali kitaalamu kama cryotherapy, matibabu ya kuua seli kwa kutumia laser na kutahiliwa kama saratani bado iko kwenye ngozi ya govi.

Matibabu katika hatua kubwa kabisa ya ugonjwa huu basi huhusisha dawa za saratani au chemotherapy, mionzi na upasuaji wa kuondoa uume kabisa na matoki yake kitaalamu kama penectomy.
Matibabu ya mionzi na dawa za saratani huweza kupunguza nguvu za kiume kwa mgonjwa ambaye uume hautaondolewa hivyo ni vizuri kujua mapema.

Njia za kuzuia saratani ya uume
Hakikisha unatailiwa na hata kabla ya kutailiwa hakikisha usafi wa uume wako.
Epuka matumizi ya sigara.
Tumia kondomu kuepuka magonjwa ya zinaa pamoja na ukimwi.

STAY ALIVE

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *