Saturday, July 27, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya ya uzazi

TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA UKENI NA MATIBABU YAKE

Uke wa kawaida wa mwanamke lazima uwe na harufu fulani, sio rahisi kusema ni harufu gani lakini wanawake huweza kutofautiana harufu hiyo. Kwakawaida uke ni nyumbani kwa bacteria wengi sana huku kukiwa na gland ambazo hutoa majimaji ya uke ambayo yana tindikali kali sana.

Kazi ya bacteria hao na glandi hizo ni kujaribu kutoa ulinzi mkali ili uke usishambuliwe na vijidudu hatarishi ambavyo huleta magonjwa. Ukiona mwanamke anapambana sana kutumia vitu mbalimbali na kufanya usafi mwingi uke wake usitoe harufu hata kidogo basi ujue anatafuta magonjwa.

Kwakawaida kuna magonjwa mawili ambayo yakianza yanakua tishio kubwa kwa mwanamke kwani huja na harufu kali kama ya kitu kilichooza na kutao uchafu wa kijani na njano, magonjwa haya kitaalamu ni bacterial vaginosisi na trichomonisis.

ugonjwa wa trichomoniasis ni upi?
huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu za siri kwa jina la trichonomiasis na husababiswa na aina ya protozoa kwa jina la trichomona vaginalis.
huu ni ugonjwa unaoshambualia angalau 10% ya wanawake wote kwenye kipindi chote cha maisha yao,
maambukizi ni kwa njia ngono kati ya mwanaume na mwanamke lakini pia kuchangia nguo za ndani au mataulo kunaweza kuambukiza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
ugonjwa huu huweza kuambukiza watu wa jinsia zote lakini unawaathiri sana wanawake na mgonjwa asipotibiwa anaweza kuishi na ugonjwa huo kwa siku miaka kadhaa.
baada ya kuambukizwa ugonjwa huu, huchukua siku 5 mpaka 28 kuanza kuonyesha dalili zake waziwazi.

dalili za ugonjwa wa trichomoniasis
kuwashwa sana sehemu za siri
kuchubuka sehemu ya juu ya uke na mlango wa uzazi
maumivu wakati wa kukojoa
maumivu wakati wa tendo la ndoa
maumivu makali ya tumbo la chini
kutokwa uchafu wa kijani na njano wenye harufu kali kama ya kitu kilicho oza.
kwa wanaume ugonjwa huu mara nyingi hauna dalili lakini mara chache sana wanaweza kupata maumivu wakati wa kukojoa

vipimo
daktari mzoefu anaweza kuujua ugonjwa huu bila vipimo vyovyote lakini pia kwa upande wa maabara uchafu unaotoka huchukuliwa na kupimwa kwa darubini…

matibabu
metronidazole au kwa jina lingine fragile 2g kwa wakati mmoja [vidonge kumi] au 400mg[vidonge viwili] kutwa mara tatu kwa siku tano.
tinidazole 2g kwa wakati mmoja
scenidazole 2g kwa wakati mmoja.
kumbuka dawa hizi hazipatani na pombe kabisa hivyo usitumie pombe ukitumia dawa hizi.

jinsi ya kuzuia
tumia kondom kila tendo na kwa usahihi
achana na ngono kama huwezi kondom
kua na mpenzi mmoja muaminifu
epuka kua na wapenzi wengi
epuka kuchangia chupi, taulo au nguo yeyote ya ndani.

Ugonjwa wa bacterial vaginosis unafanana sana dalili na ugonjwa trichomoniasis, tofauti ni kwamba chanzo chake ni kuzaliana sana kwa bacteria asilia ambao wanapatiakana kwenye uke.. chanzo kikiwa matumizi ya marashi au dawa mbalimbali za kuondoa harufu asilia ya uke, kuosha sana uke, kua na wapenzi wengi au mpenzi mpya, na kupungua kwa ulinzi asilia sehemu za siri.
Dalili, vipimo na matibabu hufanana lakini pia ni vizuri kujua kwamba kupuuzia magonjwa haya kuna madhara makubwa kama kuharibika mimba na magonjwa ya kizazi ambayo yanaweza kuleta ugumba.
STAY ALIVE

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *