Wednesday, July 24, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya ya uzazi

TATIZO LA KUTORUDIA TENDO LA NDOA BAADA YA KUFIKA KILELENI

Katika mambo ambayo yanaumiza sana vichwa wanaume walio wengi ni kushindwa kurudia tendo la ndoa kwa mara ya pili baada ya kufika mshindo kwa mara ya kwanza, wengi hudhani wana matatizo na kuanza kutafuta suluhisho ya matatizo yao kwa kutumia dawa za aina mbalimbali bila kujua kwamba wao hawana shida yeyote.

ukweli ni upi?

Kila mwanaume ana muda wake ambao anatakiwa kupumzika kabla ya kuendelea na tendo la ndoa kitaalamu kama refractory period, kuna ambao wanaweza kuendelea hapo hapo na kuna wengine wanahitaji mapumziko ya kwanzia nusu saa mpaka siku nzima.Tofauti na wanawake ambao huhitaji muda mfupi wa mapumziko au hua hawahitaji muda huu wa mapumziko kwani wao huweza kufika kileleni hata mara kumi kwa kulala na mtu mara moja kitaalamu kama multi orgasmic.

Tatizo ni nini?

Wanaume wengi hutumia muda mchache sana kufika mshindo wa kwanza kitu ambacho kinaweza kumfanya mwanamke asiridhike kwa wakati huo, sasa kwasababu mwanamke hajaridhika na anataka kuendelea basi wanaume hawa hujilazimisha kuendelea bila kupata mapumziko hayo ambayo ni ya msingi sana.Matokeo yake wanaume hawa hupaniki kwa kuhisi kwamba watapata aibu na katika kupaniki huko muda wa kurudia ndio unazidi kua mrefu zaidi.

kwanini wanaume wako tofauti kwenye jambo hili?

umri; vijana wadogo wanakua na stamina sana lakini pia mfumo wao wa damu ni msafi sana hivyo wanaweza kurudia haraka.
kuvutiwa na mwanamke; mwanaume akilala na mwanamke ambaye anavutiwa naye kingono basi ana uwezo wa kurudia mara nyingi sana kuliko akilala na mwanamke yeyote na hii nikitu muhimu sana wakati wa kuoa, hakikisha unaoa mwanamke anayekuvutia sio yeyote tu.
uwezo wa mwanamke kitandani; baadhi ya wanawake wana uwezo na utundu sana wa kukufanya utake kuendelea baada ya muda mfupi tu.
magonjwa; baadhi ya magonjwa hasa presha na kisukari huweza kuchelewesha sana muda wa kurudia tendo la ndoa.
matarajio; ukiwa na matarajio makubwa ya kuendelea na tendo lingine baada ya kumaliza tendo la ndoa kwa hofu kwamba hujamridhisha basi ndio hupati kitu kabisa.
Nini cha kufanya?
Chelewa kufika mshindo wa kwanza; ukichelewa kufika kileleni kuna uwezekano mkubwa wa kufikishwa mwanamke kileleni zaidi ya mara moja na ukajikuta unapumzika naye baada ya wewe kumaliza pia bila haraka kusubiri kuendelea mara ya pili au kutorudia kabisa kwani ameridhika.
jiweke vizuri kimwili; Fanya mazoezi mara kwa mara, hii huongeza mzunguko wa damu mwilini, hukupa stamina na uwezo wa kufanya ngono kwa muda mrefu zaidi.
tumia dawa zako kwa wakati; kama una ugonjwa wowote ambao unakuletea shida hii hasa magonjwa ya moyo, presha na sukari basji jitahidi kutumia dawa zako kwa wakati kupunguza makali ya ugonjwaa.
epuka mahusiano na mwanamke asiyekuvutia; anaweza kua hakuvutii wewe lakini kuna watu anawavutia, kua mkweli na nafsi yako na utafute mwanamke ambaye nafsi yako inaridhika naye na hapo utafurahia sana tendo la ndoa.

mwisho; mfumo wa maisha kama kunywa pombe sana, matumizi ya sigara na kupiga sana punyeto kunaweza kukufanya ushindwe kuendelea na tendo lingine kwa wakati.

STAY ALIVE

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *