Saturday, July 27, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Tiba

SINDANO MPYA ZA KUZUIA MAAMBUKIZI YA UKIMWI ZATOA MATUMAINI MAKUBWA

Shirika la ukimwi duniani, UNAIDS limepata matumaini makubwa baada ya dawa mpya ya ukimwi kwa jina la cabotegravir ambayo inatolewa kwa sindano kila baada ya miezi miwili kuzuia maambukizi ya ukimwi kuonyesha matumaini makubwa.

Utafiti huu mpya umeonyesha kwamba dawa hiyo ilifanikiwa kuzuia maambukizi kwa 89% ukilinganisha na iliyokuepo ambayo ilikua ikitolewa kwa vidonge kila siku maarufu kama PreP.

Matokeo haya ni ni muhimu sana, UNAIDS imekua ikitafuta kinga nzuri zaidi ya kuzuia maambukizi ya ukimwi hasa kwa wanawake na ugunduzi huu utakua na mchango mkubwa sana kuzuia maambukizi ya ukimwi. “Kama nchi tajiri zikiwekeza kutoa misaada na kuhakikisha watu ambao wako kwenye hatari ya maambukizi kupata sindano hizi kila baada ya miezi miwili basi kutakua na upungufu mkubwa wa maambukizi mapya”. Anaongea mkurugenzi wa UNAIDS, Winnie Byanyima.

Utafiti huu ulihusisha wanawake 3200 wenye umri wa miaka 18 mpaka 45 ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi yaani wanaojiuza na watumiaji wa madawa ya kulevya.Utafiti ulihusisha nchi za Botswana,Kenya,Malawi,Uganda na Zimbabwe. Kati ya watu 3200 waliotumia sindano ya kuzuia virusi vya ukimwi ni wanne tu walioambukizwa huku kati ya 3200 waliotumia vidonge vya kila siku watu 34 waliambukizwa.

Kwa hali kawaida yaani bila vidonge wala sindano za kuzuia maambukizi ni zaidi ya 61% huambukizwa, yaani katika watu 3200 basi watu 1952 huweza kuambuizwa nchini humo.

Shirika la ukimwi duniani linawashukuru watu wote walioshiriki kwenye ugunduzi wa dawa hizi katika mbio za kuhakikisha hakuna maambukizi mapya ya ukimwi,hakuna unyanyapaa na hakuna vifo vitokanavyo na ukimwi mpaka mwaka 2030.

Nchini Tanzania dawa za kuzuia maambukizi ya ukimwi za vidonge ambazo humezwa kila siku hutolewa katika kliniki za ukimwi lakini pia watu walioko kwenye hatari kama wanaojiuza, mashoga na watumia madawa ya kulevya hupelekewa mpaka majumbani ili kupunguza maambukizi mapya.

   STAY ALIVE

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *