Saturday, December 7, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya ya uzazi

FAHAMU JINSI UNENE NA KITAMBI UNAVYOPUNGUZA NGUVU ZA KIUME

Tunafahamu kwamba unene huambatana na magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo na kushindwa kupata usingizi wakati wa usiku lakini tatizo lingine la unene ni kupungua nguvu za kiume, kitu ambacho mara nyingi watu hawa wanene au wenye vitambi hawako wazi kukizungumzia.

Tafiti zinasemaje?

Shirika la kimarekani maarafu kama AUA au American urology association wanasema kwamba asilimia 53% ya wanaume wenye umri kati ya miaka 40 mpaka 70 wana tatizo la nguvu za kiume ambalo husababishwa na umri, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, unene na kutofanya mazoezi, uvutaji wa sigara na kiwango kidogo cha homoni za kiume yaani testosterone.

Hebu tuone uume unavyosimama.

Uume husimama pale damu inapoingia kwenye mishipa ya damu ya uume na kufanya uume ujae damu, mishipa ya damu hutoa kitu kinaitwa nitric oxide ambayo hufanya uume ubaki kwenye hali ile mpaka mwanaume atakapofika mshindo.(dawa nyingi za kuongeza nguvu za kiume huwekewa kemikali hii). Kitu chochote ambacho kinaweza kuharibu sehemu ya ndani ya mishipa ya damu ya uume husabisha uume kuishiwa nguvu.

Unene huathiri vipi nguvu za kiume?
Mtu akiwa mnene mishipa ya damu pia inakua na mafuta kwa ndani ambayo yanakua yameganda kwenye kuta za mishipa ya damu kitaalamu kama atherosclerosis, hali hii hufanya damu kupita kwa shida kwenda kwenye uume na lakini pia mfumo wa kutengeneza nitric oxide ambayo kazi yake ni kurelax misuli ya uume ili uweze kusimama unaingiliwa.

Sababu nyingine ni ongezeko la mafuta yaliyopo tumboni au kitambi ambayo hubadilisha homoni ya testosterone kua oestrogen..homoni ya testosterone ndio homoni kuu ya kiume ambayo huleta mabadiko ya yote ya kiume wakati wa kubalehe na huhusika sana na ukubwa na nguvu za kiume na kupungua kwa homoni hii humaliza au kupunguza sana nguvu za kiume.

Mwisho; habari njema ni kwamba wanaume wengi wanene huweza kurudi kwenye hali zao za zamani kwa kupungua uzito tu japokua kama ukipungua bado shida haijaisha basi kuna uwezekano mkubwa homoni zako za testosterone zilipungua na utahitaji dawa za kumeza kuzisahihisha, kumbuka kwamba kupungua uzito sio rahisi lakini ni muhimu sana.

Wengi wenu mmejaribu kupungua uzito maisha yenu yote bila mafanikio kwa kufuata diet na programu mbalimbali bila mafanikio ni vizuri sasa mkawaona wataalamu waweze kuwapa utaalamu sahihi kwa ajili ya kupungua uzito.

STAY ALIVE

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *