Thursday, May 2, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

AfyaTiba

FAHAMU CHANZO CHA TATIZO LA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA UKIWA SAFARINI.(MOTION SICKNESS)

Tatizo la kutapika kwenye safari ya gari, meli au ndege ni tatizo ambalo liko miaka mingi hata kabla ya kukua kwa teknolojia na ukisoma vitabu kigiriki na kiroma pia tatizo hilo lilionekana sana miaka hiyo. Mtu yeyote anaweza kupata tatizo hili japokua liko zaidi kwa watoto na mama wajawazito, bahati nzuri sio tatizo la kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

chanzo ni nini? Tatizo hili hutokea pale ubongo unapopata taarifa zinazochanganya kutoka kwenye mwili mmoja yaani macho yanatoa taarifa tofauti, mwili taarifa tofauti na masikio taarifa tofauti. Mfano uko kwenye ndege mwili unatoa taarifa kwenye ubongo kwamba uko unasogea lakini macho yanatoa taarifa kwamba umekaa tu lakini pia maskio ambayo yanahusika sana na kubalance usimame kwenye mstari ulionyooka yanatoa taarifa kwamba umekaa tu, na huu mchanganyiko wa taarifa au signals kwenye ubongo ndio unakufanya utapike.

dalili za hali hii.

kichefuchefu
mdomo kujaa mate
kizungungu
kutapika
mambo ya kufanya kupunguza hali hii.
pumzika na uangalie sehemu mmoja kwa muda mrefu, vuta pumzi ndefu na na epuka kupepesa macho, kufunga macho pia kunasaidia.
angalia vitu ambavyo havitembei, kama uko kwenye boti angalia mawingu na kama uko kwenye gari angalia kioo cha gari.
epuka kula kabla ya safari.
epuka kuvuta sigara wakati wa safari au harufu nzito.
epuka kunywa pombe kabla au wakati wa safari.
dawa za kutumia..
kama hii hali inakusumbua mara kwa mara basi kuna dawa zinaitwa promethazine unaweza kumeza kidonge kimoja saa moja kabla ya safari kisha ukaendelea kumeza kila baada ya nne au sita wakati safari inaendelea.
Kwa kawaida hali hii inatakiwa kuisha baada ya safari, ukiendelea kuugua baada ya safari basi huo ni ugonjwa mwingine muone daktari.

STAY ALIVE

DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
0653095635/0769846183

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *