Tuesday, October 15, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

AfyaAfya ya uzazi

FAHAMU JINSI UNENE UNAVYOWEZA KUSABABISHA UGUMBA KWA WANAWAKE

Kama wewe ni mwanamke mnene au una tumbo kubwa na umekua ukisumbuliwa na tatizo la kutobeba mimba basi ni vizuri kwanza ukaacha kuhangaika na waganga na dawa mbalimbali ambazo umeambiwa zitakusaidia na kuweka nguvu nyingi kwenye kupungua uzito.

Tafiti zinaonnyesha kwamba kadri unavyoondoka kwenye uzito wako wa kawaida yaani body mass index ya 24 ndio uwezekano wako wa kubeba mimba unazidi kua mdogo na ukiwa mnene kabisa ndio hali inazidi kua mbaya kabisa.

Mwanamke akiwa mnene au mwenye kitambi kikubwa anakua na kiwango kikubwa cha homoni inaitwa leptin ambayo hutengenezwa na mafuta yaliyoko mwilini, kiwango hichi cha homoni huingilia mfumo wa homoni za uzazi na kuuvuruga.Unene unavyozidi au tumbo linavyokua kubwa zaidi ndio hali hii inazidi kua mbaya zaidi.

Pamoja na unene kuvuruga mfumo wa homoni wanawake wanene hupata shida ya kutoa yai kitaalamu kama ovulation yaani yai linaweza lisitoke kabisa au likatoka likiwa halina ubora wa kutunga mimba hivyo huishia kuharibika.Lakini pia wanawake wa aina hii hata wakijaribu kuzaa kwa njia za kisasa yaani yai kurutubishwa nje na kupandizwa kitaalamu kama IVF bado uwezekano wa mimba kufika mwisho ni mdogo.

Dalili kuu ya hali hii ni kukosa siku zako za hedhi au kupata siku zako bila mpangilio maalumu na kwa kawaida hakuna dawa ambayo inaweza kukusaidia hapa bila ya wewe mwenyewe kuamua kupunguza uzito kwa mazoezi na chakula,

STAY ALIVE

DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

0653095635/0769846183

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *