Saturday, July 27, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

AfyaMagonjwaTiba

TATIZO LA SARATANI YA UTUMBO MKUBWA NA MATIBABU YAKE

Baada ya kifo cha mkali wa filamu za kimarekani maarufu kama wakanda au chadwick bossman kumekua na utafutaji mkubwa sana mtandaoni kujua ugonjwa huu unasababishwa na nini na ni jinsi gani mtu anaweza kukwepa ugonjwa huu.

Saratani hii huanzia kwenye sehemu ya utumbo mkubwa, mara nyingi huanza kama viuvimbe vidogo ambavyo sio saratani kitaakamu kama benign tumours au polyp lakini baadae hubadilika na kua saratani kamili na wakati mwingine hujumuisha sehemu ya mwisho kabisa ya mfumo ya chakula na kuitwa kitaalamu kama colerectal cancer. Mara nyingi ugonjwa huu huanza bila dalili na baadae dalili huanza kutokana na eneo ambalo ugonjwa umeshambulia.

Dalili za saratani ya utumbo mkubwa.

kubadilika kwa mfumo wako wa kupata choo yaani kupata choo ngumu sana au kuanza kuharisha.
maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi au kujisikia vibaya tumboni.
kupata choo chenye damu au kujisaida tamu tupu.
kujisikia kama choo haitoki yote kila ukitoka chooni.
uchovu wa mara kwa mara
kuanza kupungua uzito kwa kasi isiyo kawaida.

Chanzo cha ugonjwa huu.
Ugonjwa huu haufahamiki chanzo chake lakini inafahamika kwamba mabadiliko ya chembe za DNA ndio sababu ya saratani zote kitaalamu kama DNA mutation.
Lakini kinachofahamika kwa uhakika ni vitu ambavo vinachangia mtu kuugua ugonjwa huu kama ifuatavyo.
umri mkubwa; Saratani hii mara nyingi huwapata watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea lakini wataalamu wameanza kuona ongezeko hili kwa vijana chini ya miaka 50 na sababu hazifahamiki.
magonjwa mengine ya utumbo mkubwa; kama ushawahi kuugua magonjwa mengine ya utumbo mkubwa unaweza kua kwenye hatari ya kuugua. mfano; ulcerative colitis
mgonjwa kwenye ukoo wako; kama mzazi wako mmoja kaugua ugonjwa huu basi na wewe una hatari ya kuupata na kama kuna mtu zaidi ya mmoja kwenye ukoo wenu basi hatari ni kubwa zaidi.
chakula; ugonjwa wa huu umeonyesha kuathiri zaidi watu wanaokula sana diet ambazo asili yake ni dunia ya magharibi yaani vyakula vyenye mafuta mengi, na nyama nyingi nyekundu bila kula mboga za majani na matunda ya kutosha.
kutofanya mazoezi; watu ambao hawana tabia ya kufanya mazoezi wana hatari sana ya kuugua ugonjwa huu kuliko watu wenye tabia ya kufanya mazoezi au wanaofanya kazi ambazo zinatumia nguvu.
uzito mkubwa; watu wanene wana hatari ya kuugua na hata kufa haraka kutokana na ugonjwa huu.
sigara na pombe; watu wanaokunywa pombe sana na kuvuta sigara wana hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa huu.
mionzi; watu ambao wanapigwa na mionzi ya kupima au kutibu magonjwa fulani fulani wanakua na hatari pia ya kupata ugonjwa huu.
wagonjwa wa kisukari na watu weusi; watu hawa pia wameonyesha kuugua zaidi ugonjwa huu lakini sababu maalumu haifahamiki.

jinsi ya kutambua ugonjwa.
Colonoscopy; Hichi ni kipimo ambacho kina camera ndogo na hupitishwa kwenye njia ya haja kubwa kuangalia kama kuna uvimbe wowote wa saratani, uvimbe ukionekana basi inachukuliwa sample kwenda kupimwa maabara ili kuhakikisha kama ni saratani lakini hata kama sio saratani uvimbe huo huondolewa ili usibadilike na kua saratani.
vipimo vya damu; baadhi ya kemikali huwezwa kupimwa ili kujua kama kuna saratani mwilini mwako kitaalamu kama carcinoembryonic antigen na ukianza matibabu kipimo hichi kinaweza kugundua kama maendeleo ni mazuri mwilini mwako.

matibabu ya saratani ya utumbo mkubwa.
Matibabu makubwa ya ugonjwa huu ni upasuaji, dawa za saratani na mionzi..katika kipindi cha mwanzo kabisa cha ugonjwa huu basi mgonjwa anaweza kupona kabisa kama sehemu hiyo ya saratani ikiondolewa kwa upasuaji.
Lakini wagonjwa wengine hufika hospitali kwa kuchelewa huku saratani ikiwa ishasambaa sehemu kubwa sana ya mwili na kuifanya isitibike kabisa.

jinsi ya kujikinga na saratani ya utumbo mkubwa.
kula vizuri; mboga za majani na matunda zina vitamini fulani ambazo zina uwezo wa kuzuia saratani za aina zote kwenye mwili wa binadamu, huku afrika tuna nafasi kubwa ya kupata vitu hivi kwa bei rahisi.
kunywa pombe kiasi na achana na uvutaji wa sigara.
fanya mazoezi angalau nusu saa mara tatu kwa wiki.
kaa kwenye uzito sahihi kulingana na urefu wako.
kama uko kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu fanya vipimo kila baada ya miaka miwili au mitatu ilia kama umeanza utibiwe mapema.

 STAY ALIVE

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *