TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAUME NA MATIBABU YAKE.
Fangasi sugu za kwenye korodani za wanaume limekua moja ya matatizo sugu siku hizi za usoni, baadhi wamekua wakitumia dawa bila mfanikio yeyote na hii ni kwasababu ya kushindwa kuelewa chanzo na jinsi ya kupambana na hatari za kupata ugonjwa huu.
chanzo cha ugonjwa.
ugonjwa huu husababishwa na aina ya fangasi mwenye jina la trichopyton rubrum na waathirika wakubwa vijana,tabia kuvaa nguo za ndani zinazobana, kua mzito sana, kinga iliyoshuka kwa ukimwi, saratani, utapiamlo au kisukari, na kutokwa na jasho sana.
dalili za ugonjwa.
kuwashwa sana kwenye sana kwenye korodani.
korodani kua nyekundu hasa kwa watu weupe
korodani kuanza kutoa kama magamba kwenye ngozi.
jinsi ya kutambua ugonjwa
Daktari anaweza kutambua ugonjwa wako wa kusikiliza maelezo yako tu au kuchukua sehemu ya mabaka ya ngozi na kwenda kupima maabara,
Matibabu ya ugonjwa huu.
Kuna dawa nyingi sana za kutibu ugonjwa huu, dawa ya terbinifine ya kumeza ni moja ya dawa bora sana kwa ugonjwa huu.
Zingine ni cotrimazole, ketoconazole, gresiofulvin, na miconazole.
kumeza na kupaka kwa wakati mmoja kumeonyesha matokeoa mazuri zaidi.
Sasa jambo la msingi kabisa kuzingatia ambalo linafanya watu wengi wasipone ni kutumia dawa hizi muda mfupi, dawa hizi zinatakiwa zitumike wiki sita na sio chini ya hapo.
Mambo mengine ya kuzingatia..
kua mkavu; baada ya kuoga hakikisha umekausha mwili mzima kwa taulo safi kabla ya kuvaa nguo zingine lakini pia kausha miguu mwishoni kuzuia kuhamisha fangasi za vidoleni kwenda sehemu zingine za mwili.
vaa nguo safi: wanaume wengi wana tabia ya kuvaa nguo ya ndani moja kwa siku nyingi, jaribu kuvaa moja kila siku na kubadilisha hii itakupunguzia maambukizi yanayojirudia na hakikisha nguo za mazoezi unazitumia mara moja na kufua.
epuka nguo zinazobana sana; Vaa nguo za ndani ambazo zinakutosha ili kufanya maeneo hayo yapate hewa ya kutosha na kuepuka unyevunyevu.
usiazime nguo; epuka kuchangia taulo au nguo zako na watu wengine kwani hii itakuletea maambukizi mapya kila siku.
tibu fangas za vidole; kama una fangasi za kwenye vidole vya miguu hakikisha zinatibiwa na kupona ili kuepusha kuzisambaza mwili mzima.
STAY ALIVE