Saturday, July 27, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya ya Akili

Mtazamo kuhusu afya ya akili, hatua na matibabu vibadilike – WHO

Ripoti imetolewa leo huko Geneva, Uswisi na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO ikiwa ni tathmini kubwa zaidi kutolewa tangu kuanza kwa karne hii ya 21.

Kilichomo kwenye ripoti hiyo ni mwongozo kwa serikali, wasomi, wataalamu wa afya, mashirika ya kiraia na wengineo katika kusaidia harakati za kuleta marekebisho makubwa katika afya ya akili ambayo sasa ni tatizo kubwa.

Ukubwa wa tatizo
Mwaka 2019, takriban iwatu bilioni 1 wakiwemo asilimia 14 ya vijana wote barurbaru duniani walikuwa wanaishi na tatizo la akili.

Tatizo hilo la akili lilisababisha mtu 1 kati ya 100 kujiua na asilimia 58 ya watu kujiua ni kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 50.

WHO inasema tatizo la akili ni sababu inayoongoza ya ulemavu na watu tatizo kubwa la afya ya akili kwa wastani hufariki dunia miaka 10 hadi 20 mapema zaidi kuliko watu wa kawaida kutokana na magonjwa ya mwili yanayoweza kuzuilika.
Vichocheo vya magonjwa ya akili duniani
Ukatili wa kingono utotoni na uonevu ni sababu kubwa za msongo, halikadhalika ukosefu wa usawa kiuchumi na kijamii, dharura za afya za umma, vita na janga la tabianchi. Msongo wa mawazo na kiwewe vimeongezeka kwa asilimia 25 zaidi ikilinganishwa na mwaka wa kwanza wa janga la COVID-19.

Unyanyapaa, ubaguzi na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa watu wenye magonjwa ya akili vimesambaa kwenye jamii na kwenye mifumo ya afya: Katika nchi 20 bado jaribio la kujiua ni kosa la jinai.

Katika nchi zote, walio hohehahe na walio katika mazingira duni ambao wako hatarini zaidi kupata matatizo ya akili, ndio pia wako hatarini zaidi kutokapata huduma za kutosha.
Hata kabla ya COVID-19, ni watu wachache sana waliweza kumudu tiba ya afya ya akili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *