Friday, April 12, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

AfyaMagonjwaTiba

HAYA NDIO MAGONJWA SABA YA ZINAA YANAYOWEZA KUAMBUKIZWA KWA KULAMBA SEHEMU ZA SIRI

85% ya vijana umri wa miaka 18 mpaka 44 hushiriki aina ya ngono inayohusisha kulamba sehemu za siri au oral sex.

wengi hudhani kulamba sehemu hizo bila kushiriki tendo la ndoa huweza kuzuia magonjwa ya zinaa kitu ambacho hakina ukweli.
kwa kifupi ni kwamba;
unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa mdomoni kwako au kooni kwako kwa kulamba uume, uke au maumbile ya nyuma wa mgonjwa wa zinaa.
unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa kwa kulambwa sehemu zako za siri na mtu mwenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa mdomoni kwake au kooni.
unaweza kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa sehemu mbili kwa mpigo yaani mdomoni na sehemu za siri.
magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kwa njia ya mdomo yanaweza kusambaa mwili mzima kama yanavyosambaa haya ya kawaida.
kulamba sehemu za siri kama mkundu kunaweza kukusababishia magonjwa mengine kama ya ini na minyoo mfano hepatitis A na minyoo ya amiba.
ugonjwa wa zinaa unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu ambaye hana dalili hata moja sababu magonjwa mengi za zinaa hayana dalili kabisa.
kunyonya sehemu za siri kunaweza kuhamisha virusi fulani ambavyo hukaa sehemu za siri na kukusababishia saratani ya koo.

magonjwa yafuatayo ya zinaa huweza kuambukizwa kwa njia ya kulamba sehemu za siri au oral sex.
ugonjwa wa ukimwi; japokua hatari ya maambukizi ya ukimwi ni ndogo kwa aina hii ya ngono lakini uwezekano upo hasa kwa watu wanaotokwa na damu kwenye fidhi, wenye vidonda mdomoni au sehemu za siri, au watu wenye magonjwa ya zinaa, kwni maji maji yanayotoka sehemu za siri za mwanamke na sehemu za siri za mwanaume yanakua na virusi vingi sana vya ukimwi.

kisonono; huu ni ugonjwa unaosabbishwa na aina ya bacteria kwa jina la naisseria gonorhea, ni ugonjwa wa zinaa uliokua ukiambukizwa kwa ngono ya kawaida tu lakini tangu kuanza kutumika kwa mdomo pia ugonjwa huu unaweza kukutwa mdomoni na moja ya madhara makubwa ya ugonjwa huu ni ugumba kwa wanawake.

kaswende; huu ni ugonjwa ambao huanza na kidonda kisichokua na maumivu sehemu iliyoathirika…inaweza kua mdomoni, au sehemu za siri baadae hufuatwa na upele mwili mzima, na hata ganzi hatua za mwishoni.
ugonjwa huu hushambulia mishipa ya fahamu hivyo huweza kufika mpaka kwenye ubongo na kuleta ukichaa.

herpes; huu ni ugonjwa unaosababishwa na aina fulani ya virusi kwa jina la herpes simplex type 2, virusi hushambulia sehemu za siri za binadamu lakini vikilambwa huenda kukaa mdomoni, ugonjwa huu huweza kuambatana na virusi vya HPV ambavyo huleta saratani ya koo.


warts; hii na aina fulani ya uvimbe inayotokea sehemu za siri na huweza kuvuja damu sana kama ikijeruhuhiwa, ugonjwa huu hutibiwa kwa kuchomwa na aina fulani ya dawa au upasuaji kuuondoa sehemu husika.

Hepatitis; Huu ni mchnganyiko wa magonjwa ya ini ambayo huambukizwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kugusa majimaji au damu ya mgonjwa, kula uchafu na kadhalika.
Ni moja a magonjwa hatari sana ambayo huleta saratani ya ini ambayo kimsingi haitibiki.

chylamydia; huu ni ugonjwa wa zinaa ambao unaweza kuambukizwa kwa njia ya tendo la ndoa la kawaida au lulamba sehemu za siri.
huweza kuvamia mlango wa kizazi, kizazi chenyewe na mirija ya uzazi.

Mwisho; kulamba sehemu za siri sio mbadala wa kukimbia magonjwa ya zinaa, kama unaitaka huduma hii basi ni vizuri uwe na mpenzi mmoja ambaye ni muaminifu lakini kama una mahusiano mengi basi ni bora uwe mvaaji mzuri wa kondomu na usikubali kulamba wala kulambwa.
baadhi ya magonjwa ya zinaa hayana dalili kabisa na utakuja kujua siku unatafuta mtoto humpati.

STAY ALIVE

DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *