SABABU ZINAZOWEZA KUMFANYA MTU ASHINDWE KUENDELEA KUPUNGUA UZITO BAADA YA WIKI KADHAA ZA MWANZO.(WEIGHT LOSS PLATEAU)
Kama ushawahi kufanya mazoezi na kupunguza chakula upungue uzito utagundua kwamba mwanzoni ulipungua kwa kasi sana afu baadae ikafika hatua haupungui hata kama unaendelea na mazoezi na chakula na wakati mwingine unaona kama uzito umeongezeka kidogo. Sasa hii kitaalamu tunaita weight loss plateau ambapo ni kipindi ambacho mwili wako unakua umesimama kupungua zaidi. Sasa watu wengi wanakata tamaa yaani unatakuta mtu ana mwaka wa 2 au wa 5 yuko kwenye mazoezi na chakula lakini ana kilo zile zile.
chanzo ni nini?
Mwanzoni ukipunguza chakula mwili huanza kutumia chakula lichohifadhiwa kwenye stoo ya mwili kwenye misuli na maini yaani glycogen ambayo imetengenezwa na kiasi fulani cha maji sasa ikitumika hii uzito hupungua haraka sana. Ukianza kupungua uzito unapungua kila kitu yaani mafuta na misuli, sasa misuli huhusika na uchomaji wa mafuta pia yaani metabolism hivyo misuli ikipungua pia basi kasi ya kuchoma mafuta inapungua pia.Inafika hatua kwamba chakula unachokula japokua ni kidogo lakini kinalingana na mafuta unayochoma kwa siku maana yake hupungui zaidi ya hapo.
Nini cha kufanya?
punguza chakula: kula kiasi kidogo zaidi ya hicho unachokula kwa siku ikiwezekana robo tatu yake au hata nusu yake, hii itakufanya uchome mafuta mengi zaidi kwa siku na na kula kidogo.watu wengi hubadili diet wakifika hatua hii kitu ambacho kinawarudisha nyuma.
Fanya mazoezi zaidi; wataalamu wanashauri kufanya mazoezi nusu saa angalau mara tatu kwa wiki lakini ukifika hatua hii unatakiwa uongeze mazoezi angalau saa moja ili kuchoma mafuta zaidi.
Mambo mengine ya kuzingatia ni kuacha au kupunguza pombe, kupata uzingizi wa kutosha yaani masaa nane na kunywa maji mengi kwani yanasaidia kujisikia umeshiba muda mwingi.
Mwisho: ukifika uzito unaotaka haimaanishi kwamba ndio mwisho wa mazoezi na diet, hii inatakiwa kua sehemu ya maisha yako unaweza kula chakula unachotaka na wingi unaotaka mara moja kwa wiki lakini siku zingine unarudi kwenye diet yako na mazoezi ili kubaki kwenye uzito uleule.
STAY ALIVE