Thursday, November 21, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Tiba

HUU NDIO UKWELI KUHUSU CHANJO YA CORONA

Kumekua na mkanganyiko mkubwa sana wa maoni ya watu kuhusu chanjo mbalimbali za corona ambazo ziko sokoni sasa hivi. Baadhi ya watu wanasema chanjo hizo ni salama na wengine wanaamini kwamba chanjo hizo ni mpango maalumu wa kudhuru watu fulani na zina madhara mengi sana kwa mwili wa binadamu. Binafsi hizo naona na kama conspiracy theories kwani walalamikaji wengi wanao dai kwamba ile chanjo unawekea chip maalumu, italeta ugumba, itabadilisha seli za mwili wako na kadhalika hawana ushahidi wa kutosha wa mambo wanayosema. Lakini uwezekano mkubwa chanjo hiyo ni salama na inafaa kwa sababu zifuatazo.

Little boy is finally receiving a COVID-19 vaccine from his pediatrician

Corona imepungua au kuisha kabisa kwenye nchi zilizoendelea; Nchi nyingi zilizoendelea hasa marekani na ulaya walikua hawanga sana wa ugonjwa wa corona mwaka jana ambapo zaidi ya watu 5000 walikua wanakufa kila siku kwa kila nchi na wao ndio walifunga sana nchi zao ili kupunguza maambukizi na kusisitiza sana matumizi ya barakoa, na kunawa mikono. Dunia ya sasa inaendeshwa na kitu kinaitwa evidence based medicine yaana utatabibu wenye ushahidi, sisi wote ni mashuhuda kwamba baada ya chanjo ulaya sasa hivi wanajaza viwanja vya mpira wakiwa na mashabiki wengi bila barakoa na wakati huo huo nchi ambazo hazijapata chanjo au zilizopata chanjo kwa asilimia kidogo sana kama India zikiwa na vifo vingi sana na zingine zikirudi kwenye lockdown kama uganda na wenzake baada ya kuanza kwa wave ya tatu ya corona. Kwa lugha rahisi ni kwamba chanjo imeokoa maisha mengi ulaya.

Hakuna chanjo ambayo haina madhara; Chanjo zote zinazotolewa kwanzia utotoni mpaka kwa watu wazima sio salama kwa watu wote na baadhi zishawahi mpaka kuua watu baada ya kuchomwa sema ni kwasababu data hizo mara nyingi hakuna anayefuatilia basi kila mtu anahisi chanjo zote zilizokuepo kabla ya corona ni salama. Chanjo ya surua, kifua kikuu, donda koo, pneumonia, polio,homa ya maanjano, homa ya maini na nyingine nyingi zote zina madhara lakini madhara ya kutochomwa kwenye jamii ni makubwa kuliko madhara ya kuchomwa. Kuna dawa zingine zina madhara zaidi kuliko hiyo chanjo ya corona lakini watu wanatumia, mfano dawa ya kuzuia mimba ya P2 ina hatari wa kugandisha damu mara 10000 zaidi kuliko chanjo ya corona, sigara pia ina hatari mara 10000 zaidi ya chanjo ya corona.

Watu wanaopinga chanjo wapo hata kabla ya corona; Nchi zilizoendelea kama ulaya na marekani, hii miaka ya karibuni wametokea watu ambao wanahisi chanjo sio kitu kizuri na wameecha kuwapeleka watoto wao kunyomwa chanjo wakiamini kwamba wanaweza kuishi bila chanjo huku wakisahau kwamba kabla ya chanjo hizi, bainadamu waliishi kwa shida sana na pesa na miaka mingi sana iliwekezwa kugundua chanjo hizi. Matokeo yake kuna magonjwa ambayo yalikua yamesahaulika nchi zilizoendelea yameenza kurudi sababu ya watoto hawa.

Mwisho; Kuwa na uwezo wa kuingia youtube na google na kusoma vitu havikufanyi wewe kua mtaalamu au daktari. Kwenye internet kuna wapotoshaji wengi sana ambao kazi yao ni kutafuta attention au kuonekana kwamba na wao wana mambo ya kusema. Lakini pia mambo ya kitaalamu yanatakiwa yaachwe yafanywe na wataalamu bila kuingiliwa kisiasa kwani kuna dawa nyingi ambazo zilianzsihwa na kutumika hapa kwetu bila kua na ushahidi kama kweli zinatibu. Dawa nyingi ni sumu hata kama ni ya asili, ikitumika bila dozi maalumu huweza kuleta madhara makubwa ikiwemo kuua figo.

STAY ALIVE

 

47 thoughts on “HUU NDIO UKWELI KUHUSU CHANJO YA CORONA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *