Wednesday, February 5, 2025

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Blog

HIZI NDIO DAWA 3 ZA KUPUNGUZA UZITO AMBAZO ZIMETHIBITISHWA NA SHIRIKA LA DAWA NA CHAKULA LA MAREKANI.(FDA)

Ukiingia mtaani kuna kampuni mbalimbali kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo zinadai kuuaza virutubisho au dawa za kupunguza uzito. Lakini dawa au virutubisho vingi hua vimeandikwa kabisa “NOT FDA APROVED” maana yake kwamba wataalamu wa shirika la ubora wa marekani hawajathibitisha kweli kama hizo dawa zinafanya kazi hizo hata kama kweli kuna watu wamefaidika nazo, lakini kuna dawa chache ambazo zimefanyiwa tafiti na kukubalika na shirika hilo. Baadhi ya dawa hizo zinauzwa kwenye maduka ya madawa na zingine zinahitaji mpaka uandikiwe na daktari.

Nchini Tanzania kwa sasa kuna huduma za kupunguza uzito kwa njia za upasuaji na kuwekewa puto pale hospitali ya taifa ya Muhimbili-Mloganzila lakini sababu mbalimbali kama gharama kubwa, kutofikia vigezo na hatari ya matibabu hayo baadhi ya watu wanashindwa kutumia huduma hizo. Leo ntakuletea dawa 3 ambazo zinatumika sana hapa Marekani kwa kupunguza uzito. Kumbuka kwamba dawa hizi zinakuongezea kasi ya kupungua ukilinganisha na kupungua kwa njia ya kawaida,

Ozempic: Hii ni dawa ambayo ilitengenezwa kwa ajili ya kutibu tatizo la kisukari na dozi yake ni sindano moja kwa wiki tofauti na ile insulini ya kawaida ya kujichoma mara mbili au tatu kwa siku. Lakini dawa hii pia ilionyesha kusaidiwa wagonjwa hawa wa sukari kupungua uzito hivyo ikaanza kutumika pia na kwa watu wenye uzito mkubwa. Hii dawa kwasasa ni maarufu sana na inatumika mpaka na watu maarufu kupungua uzito. Mastaa waliokiri kutumia dawa hii ni Kim Karadashian,Teddly MellenCamp na Jameela Jamil.

Faida zake; Kupunguza uzito kwa asilimia 15-20% kwa kipindi cha miezi michache ya kwanza tu na kuiweka sukari yako sawa kwa wagonjwa wa kisukari. Ukiwa na sukari na uzito basi itapiga risasi mbili kwa wakati mmoja.

Hasara: Dawa hii ni gharama sana ikiuzwa kwanzia shilingi milioni moja na laki mbili mpaka milioni tatu kwa dozi ya mwezi mmoja tu.madhara mengine madogo madogo ni kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Ukihitaji hii dawa tunakufikishia Tanzania kwa dola 521 tu.

Phentermine topiramate; Hii ni dawa ya vidonge ambayo imethibitishwa kupunguza uzito na mamlaka za FDA. Inafanya kazi kwa kupunguza hamu ya kula. Dawa hii inapunguza uzito kwa asilimia 7 mpaka 14%.

Faida zake: Ni nzuri sana kwa ambao wanapendelea vidonge.

Madhara madogo madogo: kukosa usingizi, mdomo mkavu na madhara kwa mtoto aliyoko tumboni hivyo unatakiwa utumie na uzazi wa mpango kuepusha mimba.

Dawa hii tunakufikishia Tanzania kwa dola 200 kwa dozi ya miezi mitatu.

Orlistat; Hii ni dawa inayopunguza uzito kwa kuzuia mwili kuchukua mafuta kwenye chakula chako kwa asilimia 25%. Inapunguza uzito kwa asilimia 3 mpka 5.

faida; Inasaidia kupunguza kiasi cha cholestrol au lehemu mwilini, inapunguza presha ya damu na uzito.

Madhara madogo madogo: kutoa mafuta kwenye kinyesi na tumbo kuvuruga.

Tunakufikishia dawa hii Tanzania kwa dola 200 kwa dozi ya mwezi mmoja.

Mwisho: Kama nilivyosema hapo mwanzo ni kwamba dawa hii inaongeza kasi ya kupunguza uzito hivyo kama ulikua upungue kilo tano ndani ya muda fulani utapungua 8 au kumi lakini haimaanishi ndio ule unavyotaka. Matumizi ya dawa hizi yataambatana na muongozo wa kula, ushauri wa kitaalamu na nini cha kufanya ukipata changamoto yeyote.

Kwa wanaohitaji dawa hizi wasiliana na kampuni yetu kwa watsap namba +1(417) 324-6430 au email tanzania@w0wmedicaltz.com

 

STAY ALIVE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *