Thursday, November 21, 2024

Jifunze, Chukua Hatua Kuboresha Afya Yako

Afya ya Akili

FAHAMU TATIZO LA KUKABWA NA JINAMIZI WAKATI WA KULALA LA MATIBABU YAKE.(SLEEPING PARALYSIS)

Watafiti wa usingizi wanasema kwamba mara nyingi kuhisi unakabwa na jinamizi na kushindwa kuinua hata kidole wakati wa kulala ni dalili kwamba mwili wako umeshindwa kufuata hatua za usingizi wa utaratibu maalumu, mara chache huweza kua sababu ya magonjwa ya akili.

Kwa vizazi vingi hali hii imekua ikihusishwa sana na uchawi, majini na mashetani kwenye jamii mbalimbali na baadhi ya watu wenye imani hukemea kimoyomoyo kwa imani zao hali hii ikiwakuta lakini wataalamu wanaamini hali hii haina mahusiano na mambo giza..

Hali hii inatokeaje?

Katika hali ya kawaida wakati mtu anasinzia mwili wote hulegea kwanza na kuishiwa nguvu kisha anapotelea usingizini lakini katika hali isiyo ya kawaida mwili unalegea na kuishiwa nguvu lakini ubongo unakua bado uko macho. wakati huu unakua hujiwezi kwa chochote, unahisi kuna mtu yuko chumbani kwako, unahisi kukabwa na kusukumwa kwenda chini na unakua na hofu kubwa.

Chanzo ni nini?

Haifamiki chanzo cha moja kwa moja cha shida hii lakini huambatana na vitu vifuatavyo.

Tatizo la kukosa usingizi.
ratiba ngumu ya kulala hasa kwa watu wanofanya kazi usiku na wakati mwingine mchana mfano walinzi na wahudumu wa afya.
magonjwa ya akili.
matatizo ya wasiwasi
kumbukumbu mbaya ya siku za zamani hasa kwa wanajeshi walioenda vitani, watu waliobakwa au waliokutana na matukio magumu zamani.(PTSD).
Historia ya shida hii kwenye familia.
Matibabu
Hakuna dawa ya moja kwa moja ya kutibu hali hii lakini unaweza kutibiwa kulingana na chanzo cha tatizo kama kukosa usingizi, wasiwasi, magonjwa ya akili na kumbukumbu mbaya kwa kupewa dawa za usingizi au dawa za kupunguza msongo wa mawazo.

Jinsi ya kuzuia shida hii.
Pata usingizi wa kutosha yaani masaa 6 mpaka 8.
Fanya mazoezi mara kwa mara.
Lala muda ule ule kila siku na kuamka muda uleule.
Epuka milo mikubwa, pombe, sigara na kahawa kabla ya kulala.
usilale kwa mgongo kwani wengi hupata hii shida kwa kulala hivi
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MD
0653095635/0769846183

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *